Challenge:

Graffiti Challenge

Sura Mpya

medy maubaka


Title

Sura Mpya

Name: Artist/Group

Medy

Describe your idea (200 Words)

Katika mikoa wa Dar es Salaam, idadi ya watu inakua kwa kasi hivyo kuongeza uhaba wa viwanja vilivyopimwa na kuwalazimu wengi kujenga maeneo ambayo si salama, yanayohatarisha maisha yao. Kutokana na upungufu wa maeneo salama ya kuishi tunashuhudia wananchi wakijenga katika maeneo ambayo sio salama kwa maisha na mali zao. Moja ya eneo hatarishi ambalo watu wengi ukimbilia ni Kata ya Jangwani ambayo kwa mujibu wa Sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, Kata ya Jangwani ina wakazi wapatao 15,722 ambao wanaongezeka kwa kasi ikikadiriwa kuwa na wakazi 20,000. Katika maeneno ya Jangwani watu wengi hujenga kwenye vyanzo vya maji, kando ya mto bonde la Msimbazi kiasi kwamba mvua ikinyesha wanakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na maafa. Serikali kwa kushirikiana na wadau tofauti imekua ikitoa misaada kwa waathirika na kuwataka kuhamia maeneo salama, ambayo wakati mwingine hutengwa kwa ajili yao, bila mafanikio. Kwa kufahamu hilo mchoro huu unalenga kuonyesha sura mpya ya ujenzi unao zingatia Sheria za Mazingira na Mipango Miji. Unachoro unaonyesha ubora na faida ya kuwa na mji uliyopangiliwa ukiwa na makazi salama pamoja na miundo mbinu bora kwa ustawi bora wa jamii zetu. Huu ni wakati wa kila mtendaji kuangalia uwezekano wa kuboresha makazi kwa wananchi wake ili kupunguza majanga yanayotokana na ujenzi holela.

Project Tagline

Makazi Salama sio ndoto

Comments