Challenge:

Graffiti Challenge

Leo Kesho

Mawila Khamsini (localfanatics)


Title

Leo Kesho

Name: Artist/Group

LocalFanatics

Describe your idea (200 Words)

Dar es salaam ni kati ya jiji lenye mafanikio makubwa na Dar ni jiji lililo bahatika kuwa karibu na vyombo vya dola na serikali. Pasipokuwa uhalisia ni kuwa Dar es Salaam ina maeneno ambayo sio salama kuishi, suala la miundombinu mibovu ya barabara, maji, umeme na mpangilio mbaya wa jiji vinahatarisha usalama wa jiji kwa kiasi kikubwa. Moja ya maeneo yanayoathiriwa na majanga yanayotokana na mipango mibovu ya dharura ni pamoja na Kata ya Jangwani,wilaya ya Ilala. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata hii ina wakazi wapatao 15,722 waishio humo. Kutokana na ufahamu huo; mchoro huu imejikita kushirikisha wadau wa kijamii wakiwemo Serikali ya Wilaya, Mkoa, Wananchi, asasi za kiraia kushirikiana na Idara ya mipango mji kuhakikisha kuwa kuna mikakati mbalimbali yakiwamo uandaaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi, kufanya uthamini wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiwajibika na kuikumbusha Serikali kutia mkazo kwenye miradi ya upimaji viwanja kwa ajili ya maeneo ya huduma mbalimbali na maeneo ya umma. Mipango miji ndio wenye dhamana kubwa kuhakikisha ukuaji wa miji yetu ni salama kwa wakazi, lazima maeneo ya wazi na ya barabara yaheshimiwe, mikondo ya maji ya asili isizuiliwe kwa ujenzi holela, mifumo ya bora ya dharura ikiboreshwa majanga kama mtoto yataweza kuthibitiwa kwa kuwa na miundo mbinu bora inayosaidia maeneo kufikika wakati wa ajali au dharura. Mchoro huu pia unahamasisha juhudi shirikishi, Serikali pekee haitoshi. Suala la usalama wa jamii zetu upo mikononi mwetu sote. Kwa kuhakikisha tuna utii wa sheria kama Sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, Sheria ya Ardhi na Mipango miji basi kutakuwa na uwepesi wa kuthibiti majanga ndani ya jamii zetu.

Project Tagline

Mipango Salama

Comments