Challenge:

Graffiti Challenge

Tuanze Sasa

Elias Biya


Title

Tuanze Sasa

Name: Artist/Group

Elias Biya

Describe your idea (200 Words)

Miaka baada ya miaka watu wamekua wakitafuta ajira na maisha bora mijini. Inakadiriwa kufikia mwaka 2050 watu 7 kati ya 10 wataishi mijini. Lakini miji mingi hukabiliwa na majanga kama vile mafuriko na majanga mengine ya asili. Mabadiliko ya hali ya hewa yamefanya mambo kua mabaya hata zaidi. Kati ya majanga ayo mafuriko ndio uwaathiri watu wengi zaidi. Hapa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mafuriko yamekua ni janga kubwa. Eneo la jangwani limekua likisumbuliwa sana na tatizo hili japo kuna maeneo mengi pia yanapata shida hii. Mwaka 2016 katika daftari la wapiga kura ilionyesha jangwani kuna zaidi ya wakazi 22,098 kati yao ni 500 tu wenye vibali halali. Ujenzi wa makazi kiholela ni sababu kubwa ya mafuriko kuwa tatizo sugu eneo la jangwani. Mengi yanahitaji kufanyika ili kuzuia na kupunguza hatari kabla ya janga lingine la mafuriko halijatokea. Mfano kujenga miundombinu imara na yakutosha na pia wananchi kufata ramani za kiserikali wanapotaka kujenga makazi na pia kupanda bustani na miti kutapunguza madhara ya mafuriko au hata kuzuia uwezekano wa kutokea mafuriko. Katika mchoro wangu nimeonyesha jinsi gani wananchi na serikali wanaweza kushirikiana kutengeneza jiji stahmala. Tuanze sasa.

Project Tagline

Wakati ujao uliothabiti.

Comments

  • ISACK AMINI13th, August 2018

    Great mind. I love your passion and vision of the city.RESPECT.