Challenge:

Graffiti Challenge

Maisha ni Sasa

hafidh athuman


Title

Maisha ni Sasa

Name: Artist/Group

Kalasinga

Describe your idea (200 Words)

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, Kata ya Jangwani ina wakazi wapatao 15,722 waishio humo. Katika maeneo ya Kata hii baadhi ya nyumba au majumba ujenzi wake katika miaka ya karibuni hauzingatii umuhimu wa kuchimba mashimo ya kuhifadhia maji taka. Wakazi wengi wa maeneo haya hukwepa gharama za ujenzi wa mashimo ya maji taka pasipo kuzingatia madhara yake. Kutokuwepo kwa mashimo ya maji taka pamoja na huduma za magari tosha ya maji taka yamepelekea na kusababisha maji taka kumwagwa ovyo barabarani hata kuwa moja ya vyanzo vya kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindupindu. Kupitia mchoro huu ni muhimu kuhamasisha hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa kuanza na wajenzi wa nyumba ambao hawazingatii kujenga mashimo ya kuhifadhia majitaka. Uboreshwaji wa mifumo ya magari ya maji taka na miundo mbinu stahiki ya umwagaji maji taka utapunguza janga la magonjwa la milipuko. Ni muhimu sote tukisimama na kuhakikishe kuwekwa ama kujenga mfumo wa maji taka utakaowalazimu wanaohudumiwa na mfumo huo kuulipia kila baada ya muda fulani kwa kiwango shirikishi kwa lengo la kuwezesha ujenzi wa miundo mbinu bora (Chemba).

Project Tagline

Linda Maisha, maji taka sio poa.

Comments