Challenge:

Graffiti Challenge

MFUMO WA MAJI TAKA

Ramadhani Mabera


Title

MFUMO WA MAJI TAKA

Name: Artist/Group

Ramadhan mabera

Describe your idea (200 Words)

Maeneo mengi ya Dar-es-salaam hasa kipindi cha mvua kumetokea na tabia ya wakazi kutapisha maji taka,hii inatokana na mfumo mbaya wa maji taka. Kutokana na taarifa zilizotolewa na gazeti la mwananchi la tarehe 30 may 2018 limesema kwamba wakati serikali ikikusudia kuanzisha mradi wa usafishaji wa maji taka jijini Dar es salaam,imebainika kuwa asilimia 90 ya wakazi wa jiji hilo hawana huduma ya maji taka hali inayoashiria uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo oevu kinyume na sheria ya usimamizi wa mazingira. Kutokana na taarifa iliyotolewa hapo juu mlengwa haswa anayekusudiwa ni mkazi wa Dar es salaam hususani yule anayeishi maeneo ya mabonden Ili juhudi za kuliondoa tatizo hili liweze kufanyika ,inahitajika msaada mkubwa kutoka kwa serikali ,wanajamii na mashirika ndani na nje ya Tanzania. Hivyo basi suruhisho la tatizo hili ni kuwepo kwa magari yatakayo beba maji taka na vilevile pia kuwepo pia kuwepo kwa ujenzi wa mifeleji katika mitaa mbali mbali ndani ya jiji la Dar es salaam. Kutokana na tabia hii ya wakazi wa Dar es saam kutapisha maji taka haswa kipindi cha mvua na kupekekea kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.Hivyo naiomba serikali iwe na idadi sahihi kwa wakazi sahii, miundo mbinu bora na makazi salama kwa wakazi wote. Kutokana na changamoto wanazozipata wakazi wa dar es salaam hususan wanaoishi mabonden ningependa serikali iwapatie suruhisho ili waepuka magonjwa ya mlipuko na janga la mafuliko.

Project Tagline

Comments