Challenge:

Graffiti Challenge

Mazingira safi na salama

Mariam Oushoudada


Title

Mazingira safi na salama

Name: Artist/Group

Mariam Oushoudada

Describe your idea (200 Words)

Wakati wa mvua wakazi wa Jangwani na wakazi wengine wa Dar es Salaam huona ni fursa ya kutupa uchafu kwenye mifereji ambayo matakataka hayo huishia kusombwa na mto msimbazi na kulundikana pembezoni mwa mto msimbazi maeneo ya jangwani inayopelekea hali hatarishi za magonjwa kama cholera kwa watoto wanaocheza karibu na mto huo. Kutokana na mafuriko hayo watoto watano wameripotiwa kufa jangwani.(www.bbc.com2014) Wakazi wa jangwani kama inavyoelezwa na Bi Charemebe ambaye ni mkuu wa serikali za mitaa Jangwani alieleza pia vyombo na vitu vya ndani vya wakazi wa jangwani huelea kwenye mto ambacho ni chanzo kingine kinacholeta maafa kwa watoto.(www.Tanzaniatoday.com). Watu ninaotazamia kuwalenga ni wakazi wa Jangwani na wadau wangu wakiwa wanafunzi, Serikali, Wasanii na Asasi zisizozakiserikali kwasababu hawa wana uwanja mkubwa wakufundisha wengine na mwishowe kufikia hata Tanzania nzima. Agenda yangu ni kuelimisha wadau hawa kuhusu usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko hasa kwa watoto na kupelekea mazingira safi na salama. Ninajali mazingira kuwa salama hususan ya Jangwani kwasababu ningependa kuona vizazi vinavyofuata vinakuwa katika mazingira salama yatakayowapelekea wafikie ndoto zao ambazo zitakuza na kupendendezesha jamii.

Project Tagline

Mazingira Safi ni Maisha Salama

Comments