Challenge:

Graffiti Challenge

PAMOJA TUNAWEZA KULETA MABADILIKO

beatrice mashala


Title

PAMOJA TUNAWEZA KULETA MABADILIKO

Name: Artist/Group

BEATRICE MASHALA

Describe your idea (200 Words)

UJUMBE ; Uboreshwaji wa makazi ya Jangwani yawe safi na salama kwa wakazi husika na wapita njia. Jangwani ni eneo ambalo liko manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam . TAARIFA kwa mujibu wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2012 Jangwani ilikuwa na wakazi wapatao 15,722 na Mwaka 2016 wakazi 22,098 huku wakazi wenye leseni halali ni 500 na asilimia 80 wakiwa hawana leseni za makazi , kwahiyo wanaishi kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. WALENGWA ; ni wakazi wa Dar Es Salaam na kupitia mchoro huu utakaochorwa katika kuta ambayo hupitisha wakazi takriban laki 250.000 kwa siku itakuwa njia sahihi kufikisha ujumbe kwa walengwa. WADAU ; SERIKALI ambao ndio watekelezaji wakuu wa miradi katika jamii mashirika binafsi , watu binafsi , mashirika ya kimataifa asasi zisizo za kiserikali kwa ujumla watasaidia kifedha , kuelimisha jamii kuhusu mazingira salama. AGENDA ; kushawishi na kuleta mabadiliko kwenye makazi ya jangwani yawe salama na stahamala kwa wakazi husika na wapita njia. WITO ; Makazi sahihi kwa miundombinu bora. KWANINI UNAJALI ; Kwasababu wakazi husika wanaishi katika mazingira hatarishi ( hususani mustakabali wa watotot wanaoishi eneo hili ambalo sio rafiki kwao ) na stahamala kwahiyo yanaathiri uchumi wao, afya na elimu na nyanja zote za maisha yao.

Project Tagline

MAKAZI SAHIHI KWA MIUNDOMBINU BORA

Comments