Challenge:

Graffiti Challenge

Kwa Pamoja Tutaweza.

Joseph S Mdamanyi


Title

Kwa Pamoja Tutaweza.

Name: Artist/Group

Joseph S Mdamanyi

Describe your idea (200 Words)

Taarifa: Kutokana na vyanzo mbalimabali ikiwemo wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, kata ya Jangwani iliyopo katika manispaa ya Ilala, imekua na idadi kubwa ya wakazi kuliko uwezo wa eneo wa kustahimili. Kutokana na takwimu za sensa ya mwaka 2002 kata ya jangwani ilikua na idadi ya wakazi takriban 15722, lakini kufikia mwaka 2016 imekua na wakazi takriban 22098. Pamoja na idadi ya wakazi kuongezeka kwa kiasi kikubwa kiasi hiki, ni wakazi takriban 500 pekee ndio wenye leseni za maeneo yao. Na hii imepelekea kuwa na asilimia 80% ya wakazi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Mlengwa: Mkazi wa jiji la Dar es Salaam Wadau: Serikali, Asasi zisizo za kiserekali, Watu binafsi, Wasanii, Wafanyabiashara, Agenda: Ushirikishwaji wa watu mbalimbali katika kutekeleza wajibu wa kuijenga Dar es Salaam Stahmala. Wito: kwa pamoja tutengeneze jamii isiyotegemea serikali katika utekelezaji wa sera maendeleo hususan zinazohusu utunzaji wa mazingira, bali ushirikiano madhubuti kati ya serikali na jamiiyote kwa ujumla ili tuweze kuifikia Dar es Salaam Stahmala. Kwa nini najali: Mimi kama Mtanzania, Mwana mazingira na msanii, kwa namna zote hizi, mimi ni muhusika moja kwa moja katika kuijenga Dar es Salaam Stahmala.

Project Tagline

Sote ni wajibu wetu kuijenga Dar es salaam stahmala

Comments